Risper ni mojawapo ya socialites wanauvuma sana Kenya. Kwenye moja wapo ya video zinazotamba mtandaoni, anaelezea wanawake kutumia maujanja kupata pesa kwa wanaume.
Anaelezea alivyo tumia kisa cha ajali iliyo tokea pale Nakuru kutengeneza pesa kutoka kwa wanaume wanaommezea. Alikuwa anaelekea kwa mkutano ya watu wa Rugby pale Nakuru. Kulingana na maelezo yake, Risper Faith alisimamisha gari lake karibu na eneo la ajali ili apige picha zake swafi. Picha zenyewe zilikuwa zapigwa kiujanja ndo itokeze kama Risper alikuwa amehusika ile ajali.
“Tupata gari iliyokuwa imepata ajali ikiwa bado na damu damu pale. Nilipaka ile damu usoni kisha nikapiga picha ambazo nilitumia wanaume 30 ambao najua huwa wananitaka,” socialite alisema.
Risper Faith anaendelea kusema katika harakati za kupiga picha, aliona hospitali karibu. Pale ndani alikutana na daktari flani akampa Ksh 3,000 ndo amsaidie kufaulisha ile utapeli. Daktari yule alimsaidia kufika emergency department ambapo alipiga picha zaidi iliionekane vile alikuwa ameumia.
“nilifanya mpango na daktari mmoja pale hospitalini nikalazwa kiandani nakuwekewa oxygen,” alieleza Risper Faith.
Aliendelea kusema kwamba picha zote zilitumiwa wanaume 30 waliokuwa wanammezea. Pia aliwaelezea bill ya hospitali ilikuwa Ksh 56,000 ndo wamtumie msaada.
Baada ya kupiga picha na kutumia wale wanaume 30, Rispa aliendelea na safari yake hadi kwa ile Rugbi event. Anasema, in total, wanaume wale walimtumia Ksh. 256,000.